Shabani Ramadhani

 

Shabani Ramadhani ni Mwenyekiti wa kikundi cha Social Vision kikundi cha ushirika wa kilimo cha Mbogamboga kilichopo Mtaa wa Maisaka Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.

 

Mahali: Babati, Manyara, Tanzania

Simu: 0712-306840

Barua pepe: shabanrama565@gmail.com  

 

TAARIFA ZA KIBIASHARA

Kikundi cha Social Vision ni kikundi cha ushirika wa kilimo cha Mbogamboga chenye wanachama watano (5), kilichojikita katika uzalishaji wa miche bora na mazao ya mbogamboga kwa watumiaji wa kaya zinazowazunguka.

 

Shabani Ramadhani ni Mwenyekiti wa kikundi cha Social Vision. Kwa sasa zaidi ya ekari moja na nusu ya shamba lao wamelima mazao kama vile nyanya pilipili, mboga za majani aina zote na vitunguu.

 

Ndg Shabani Ramadhani na kikundi chao wana mpango kupanua na kukuza kilimo chao cha uzalishaji miche ya mboga mboga kwa ajili ya matumizi yao shambani na kwa ajili ya biashara ya uuzaji kwa wakulima wengine.

 

Kwa mujibu wa Ndg Shabani Ramadhani kuwa mwanachama wa TCCIA – Manyara kumewanufaisha sana na kuwa na umuhimu hasa katika utafutaji na upatikanaji wa masoko ya ya biashara ya mazao yao. Uanachama wao TCCIA umewawezesha kupata Mafunzo ya Uendelezaji Biashara (BDS Service) kuungana na kujuana na wakulima wengine na wadau mbalimbali ambao umepelekea kukua kwa biashara yao ya uzalishaji wa miche na mbogamboga


 

 

 

 

 

 

 


 

 

Shabani Ramadhani

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Shabani Seedlings

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Shabani drip irrigation