Training 1

 Shughuli / Huduma za TCCIA

 • Majadiliano/ Ushawishi & Utetezi
 • Habari za Biashara
 • Watafutaji Ubia
 • Maonyesho ya Biashara / Ziara za Kibiashara
 • Mafunzo / Makongamano
 • Vyeti vya uasili (Certificate of Origin)
 • Urasimishaji wa biashara.
 • Ushauri wa Biashara
 • Huduma za Uhazili
 • Uchambuzi yakinifu wa Kisekta / Kutengeneza hiifadhidata (Database)
 • Mafunzo ya ujasiriamali kwa ujumla.
 • Mafunzo ya VICOBA

 

MAJADILIANO/UTETEZI & USHAWISHI

TCCIA ni msemaji mkuu wa jumuiya ya wafanyabiashara nchi nzima. Inafanya ushawishi kupitia serikali vyombo vya habari na asasi zote za hapa nchini na za kimataifa ambazo shughuli zake kwa namna moja ama nyingine huathiri Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania. Ushawishi huo unafanyika kwa ngazi ya kitaifa , kimkoa au kiwilaya kwa kutegemea ukubwa wa tatizo. Kwa sasa TCCIA ndio sauti pekee ya watu wote wanaojishughulisha na biashara  wawe wakubwa au wadogo.

 

HUDUMA ZA TAARIFA ZA BIASHARA

TCCIA ina vituo vya taarifa za biashara katika chemba zote za mikoa pamoja na makao makuu mjini Dar es Salaam. Vipo vitabu vyenye majina anwani na habari mbalimbali za biashara. Pia kuna orodha ya majina na mahali bidhaa zinapopatikana  na kuhitajiwa. Vipo vipeperushi, majarida na machapisho mbalimbali ya biashara ambavyo humpa muagizaji wa bidhaa na anayeuza nje taarifa muhimu zinazohusiana na  biashara za kimataifa.TCCIA inapokea maombi mengi ya biashara kutoka duniani kote . Kampuni zinazotafuta wateja  au wasambazaji hutuma maombi yao kupitia mtandao  unaoaminika wa TCCIA. Maombi hayo huchapishwa kwenye tovuti yetu www.tccia.com na kwenye taarifa na majarida yetu.

 

WATAFUTAJI UBIA

Tafuta wabia (Business Partners) kwenye hifadhidata (database) za hapa nchini na za kimataifa ikiwa ni pamoja na hifadhidata ya compass (Kompass Database) yenye maelezo ya kampuni milioni 1.8 kutoka nchi 75, majina na alama za biashara 704,000 na majina ya watendaji wakuu wa makampuni milioni 3.5.

 

MAONYESHO YA BIASHARA / ZIARA ZA KIBIASHARA

TCCIA inatoa fursa kwa wanachama wake kutangaza bidhaa zao kwa kuendesha maonyesho ya biashara mara kwa mara ndani na nje ya ya nchi.Chemba pia inatuma na kupokea jumbe za biashara kutoka nchi mbalimbali. Hii inamwezesha mwanachama wa chemba kuonana na wabia wa kimataifa na kupanua uwezo wa kibiashara.

 

MAFUNZO / MAKONGAMANO

TCCIA inachambua mahitaji ya jumuiya ya wafanyabiashara na kupanga mikakati ya kuitanzua.Hutoa mafunzo na kuendesha makongamano kwa wanachama wake juu ya stadi za biashara, utozwaji kodi, mauzo , masoko  na namna ya kutafuta taarifa za biashara . Pia hutoa mafunzo ya teknolojia ya biashara na uhasibu.

 

VYETI VYA BIASHARA (CERTIFICATE OF ORIGIN)

TCCIA ambayo ni chemba kubwa kuliko zote iliyoanzishwa kwa ajili ya kuisaidia sekta binafsi ndiyo pekee inayoruhusiwa kutoa vyeti nchini Tanzania vinavyoonyesha wapi bidhaa zinatoka .Inatoa vyeti vya aina saba. Vyeti vya biashara ya kimataifa (ICC), COMESA. SADC, SACU-MMTZ,EURI,AGOA na GSP

 

MAHUSIANO

TCCIA ni mwanachama mshiriki wa asasi nyingi za ndani na nje ya nchi kama vile EAC,SADC,COMESA na ICC pamoja na Chemba za Afrika na ng’ambo ambazo imewekeana makubaliano ya kushirikiana.Makubaliano haya yanaiweka TCCIA kwenye ramani ya dunia ya biashara.

 

USHAURI WA BIASHARA

TCCIA ina timu ya wafanyakazi wenye sifa ambazo wanatoa ushauri juu ya mambo ya biashara,viwanda na kilimo.

 

HUDUMA ZA UHAZILI

 • TCCIA inatoa huduma za uhazili na wavuti (internet) katika chemba za mikoa na matawi ya wilayani. Hudma nyingine inazotoa ni
 • Kuandika barua na kupiga chapa
 • Kurudusu (photocopying) na kuunganisha (binding)
 • Huduma za simu, faksi na barua pepe
 • Huduma za kutafuta taarifa kwenye wavuti (internet)
 • Kuchora kwa kutumia kompyuta, kutayarisha kadi za biashara na kutoa karatasi ambazo zina anwani (letter heads
 • Kutengeneza tovuti