Kuhusuoffice

TCCIA Logo Banner            

 

 

Chama cha Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Tanzania kilianzishwa mwaka 1988 kwa msaada wa serikali ya Tanzania, ikiwa na lengo la kuunga mkono uchumi wa kikanda na maendeleo ya makampuni mbalimbali ya sekta binafsi na mashamba. TCCIA imeanzisha ofisi za kikanda 21 na kila mkoa ni huru katika shughuli zake za uendeshaji.

DIRA

“Kuwa taasisi inayoongoza kwa kuweka mazingira bora ya kibiashara kwa wanachama wake katika Mkoa wa Manyara.

DHAMIRA

“Kuunda mtandao imara wa asasi zinazomilikiwa na  wanachama kwa kutoa taarifa za kibiashara, mafunzo ya ujasiriamali, ushawishi na utetezi ili kuwezesha mazingira bora na endelevu ya kibiashara”.

 

 

 

Ujumbe kutoka kwa mwenyekiti

 

TCCIA Logo Banner

Mkoa wa Manyara ni moja ya mikoa 30 ya utawala Tanzania. Mji mkuu wa mkoa wa Manyara ni Babati Mjini. Mkoa huu una wilaya kuu 5 yaani Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto na Hanang’. TCCIA Manyara mkoa ilianzishwa mwaka 2004 ikiwa na wanachama 96. Kwa sasa TCCIA Manyara ina wanachama wapatao 913. Makao makuu ya TCCIA Manyara yapo Babati mjini. Kabla ya kuanzishwa kwa TCCIA Manyara wanachama walihudumiwa na TCCIA Arusha kabla ya mkoa mama wa Arusha kugawanywa na kuuunda mikoa miwili ya Arusha na Manyara.

TCCIA Manyara ni chombo kinachounganisha jamii ya wafanyabiashara katika ngazi ya mkoa. TCCIA ina nia ya mabadiliko endelevu, kutoa ushauri na utetezi, kukuza mahusiano ya biashara ndani ya jamii ya wafanyabiashara pamoja na serikali, nah ii ni kusaidia kuweka usawa katika maadili ya kiashara, kukuza, kuratibu na kulinda maslahi ya uchumi wa kibiashara katika sekta mbalimbali za uchumi hasa sekta ya viwanda, biashara na kilimo ili kukusanya na kusambaza taarifa za kibiashara na uchumi kwa ujumla ndani ya mkoa.

Shukrani maalum ziende kwa TRIAS Tanzania kwa msaada endelevu kwa shughuli za TCCIA Manyara, usimamizi na wanachama. Juhudi zao zimewezesha Bodi kutekeza majukumu yao vizuri. Shukrani pia ziende kwa Word University Services of Canada (WUSCA) kupitia program ya UNITERRA kwa kudhamini uzinduzi na utengenezaji wa tovuti hii.

Shukrani nyingine ziende kwa mashirika na vyama ambavyo TCCIA Manyara inashirikiana navyo; TCCIA Arusha, MVIWATA Manyara, FIDE, MACSNET na SIDO Manyara.

Asante.

Karibu TCCIA Manyara

Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Manyara.

     

 

 

 

  

 

Chairman

Ujumbe wa ukaribisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi,  Mr. Stanley Mchome.

 

 

 

 

 

 

Wageni